» » Maalim Seif azipiga kufuli akaunti za CUF, Lipumba Alalamika

Maalim Seif azipiga kufuli akaunti za CUF, Lipumba Alalamika

Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama Siasa, Prof. Ibrahim Lipumba amelalamikia kitendo cha Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharrif Hamad kuzifunga  akaunti zote za chama hicho za wilaya.
 
Ameyasema hayo wakati wa kikao cha baraza la uongozi linaloongozwa na upande wake. Profesa Lipumba amesema kutokana na uamuzi huo ruzuku ya chama kutoka serikalini wameikosa.
 
“Wajumbe nawashukuru kwa kuja ili kupata fursa ya kujenga chama. Chama chetu kipo ndani ya mtihani ambao kwa kweli chanzo chake ni Katibu Mkuu wetu kutoheshimu katiba yetu na kutoheshimu taratibu za kidemokrasia,” amesema Prof. Lipumba.
 
Aidha, Prof. Lipumba amesema kuwa Maalim Seif alitakiwa kuhudhuria kikao hicho na alipewa taarifa lakini hakuweza kufika, hali iliyosababisha majukumu yake kusimamiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara. Magdalena Sakaaya.
 
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Zanzibar), Nassor Mazrui amesema kuwa hatua ya kufunga akaunti za benki imelenga kulinda fedha ya chama ili zisitumiwe vibaya na upande wa Profesa Lipumba.
 
Hata hivyo, Msajili wa Vyama vya Siasa bado anamtambua Prof. Lipumba kuwa ni Mwenyekiti wa chama hicho kwa kuwa hakuwa na taarifa kuhusu uamuzi wake wa kujiuzulu.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440



BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en





tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...