Mkurugenzi wa FBI apinga madai ya Trump kuhusu Obama
Mkurugenzi wa shirika la kijasusi la FBI James Comey amekana madai ya rais Donald Trump kwamba aliyekuwa rais wa taifa hilo Barrack Obama alidukua simu yake kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.
Bwana Comey amesema kuwa amelitaka shirika la haki nchini humo kukataa madai hayo kwamba Obama aliagiza uchunguzi wa simu za Donald Trump wakati wa kampeni za uchaguzi uliokwisha.
Alikana madai hayo akisema kuwa yanayoonyesha FBI ilivunja sheria.
Hatua hiyo iliripotiwa na gazeti la the New York Times na kuthibitishwa na NBC.
Idara ya haki haikutoa taarifa ya mara moja kuhusu ombi la bwana Comey.
Vyombo vya habari nchini Marekani viliwanukuu maafisa vikisema kuwa bwana Comey anaamini hakukuwa na ushahidi kuthibitisha madai ya Trump.
Rais huyo wa chama cha Republican ambaye anakabiliwa na uchunguzi mkali kuhusu uingiliaji wa Urusi ili kuunga mkono uchaguzi wake hajatoa ushahidi wowote kuunga mkono madai yake kwamba simu zake katika ofisi ya Trump Tower zilidukuliwa.
BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment