Mji wa Durban hautandaa Mashindano ya Madola mwaka 2022
Haki miliki ya pichaREX FEATURESImage captionDurban ungekuwa mji wa kwanza barani Afrika kuandaa mashindano hayo mwaka 2022.
Mashindano ya Madola ya mwaka 2012 hayatafanyika tena nchini Afrika Kusini mjini Durban nchini Afrika Kuisini, BBC imebaini.
Inaaminiwa kuwa mji huo haukutimiza viwango vya shirikisho la mashindano ya Madola na tangazo linatarajiwa kutolewa baadaye leo.
Durban ilipewa nafasi hiyo mwaka 2015 kama mji pekee uliotuma ombi na ungekuwa mji wa kwanza barani Afrika kuandaa mashindano hayo.
Mji wa Liverpool nao ulikuwa umeonyesha dalili ya kutaka kuandaa mashindano hayo.
Mashindano ya Madola yalifanyika kwanza mwaka 1930 na hufanyika baada ya kila miaka minne na kuwaleta pamoja wanariadha kutoka zaidi ya nchi 50 hususan zilizokuwa koloni za Uingereza.
Mwezi uliopita waziri wa michezo wa Afrika Kusini Fikile Mbalula, aliashiria kuwa huenda mji huo ukandaa mashindano hayo kutokana na changamoto za kiuchumi.
Mshirikishe mwenzako
No comments:
Post a Comment