Marekani kuanzisha uchunguzi kwa mashambulizi ya Mosul,Iraq
Image captionMapigano yanayoendelea Mosul yamesababisha mamia ya watu kufariki ukiachilia mbali kupoteza makazi yao
Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema kuwa inaanzisha uchunguzi juu ya tuhuma za ndege za nchi hiyo kushambulia wananchi wasiokuwa na hatia katika mji wa Mosul nchini Iraq mapema mwezi huu.
Katika kulishughulikia jambo hilo, zaidi ya mikanda ya video mia saba itachunguzwa.
Msemaji wa jeshi la Marekani kanali J T Thomas amesema kuwa jeshi la nchi hiyo lilifanya mashambulizi karibu na eneo hilo lakini hawakulifikia.
Ameongeza kuwa hakuna mabadiliko katika kupambana na vikosi vya IS na hawatarudi nyuma.
Mshirikishe mwenzako
No comments:
Post a Comment