» » Manchester United watawakosa Chris Smalling na Phil Jones muda mrefu

Manchester United watawakosa Chris Smalling na Phil Jones muda mrefu

Hivi ni viunganisho vya nje na vitafungua katika dirisha mpyaSambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Messenger Sambaza habari hii Email Mshirikishe mwenzako

Haki miliki ya pichaEMPICSImage captionPhil Jones (pili kushoto) anaonekana kuumia baada ya kukabiliwa na Chris Smalling (kati) wakati wa mazoezi

Mabeki wa Manchester United Chris Smalling na Phil Jones walipata majeraha ya kuwaweka nje kwa muda mrefu walipokuwa wanachezea timu ya taifa ya England, meneja wa klabu hiyo Jose Mourinho amesema.

Jones, 25, aliumia kwenye kidole wakati wa mazoezi akikabana na mpinzani.

Taarifa zinasema kisa hicho kilimhusisha Smalling.

Beki mwenzake Smalling, 27, alipigwa picha akiwa amefungwa kitambaa mguuni baada ya kuumia pia wakati wa mazoezi.

'Yuda' Mourinho 'bado anaongoza Chelsea'

Nahodha wa United Wayne Rooney hata hivyo amepata nafuuu na atarejea kuwachezea dhidi ya West Brom Jumamosi baada ya kupona jeraha la goti.

Rooney, 31, alikosa mechi United za karibuni zaidi walizocheza United.

Kutokana na kuumia kwa Smalling na Jones, Mourinho amemwita beki wa miaka 19 Axel Tuanzebe kikosini kwa ajili ya mechi hiyo.

Tuanzebe amechezea United mechi moja pekee ya ushindani, mechi ambayo walilaza Wigan 4-0 katika Kombe la FA Januari.

United watakuwa pia bila mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic na kiungo wa kati Ander Herrera wanaoumikia marufuku.

Pia, watamkosa Paul Pogba, anayeuguza jeraha la misuli ya paja.

Mada zinazohusiana

UingerezaMichezoKandanda

Mshirikishe mwenzako 

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles