Malaysia yawafukuza watu 50 raia wa Korea Kaskazini
Malaysia inasema kuwa itawafukuza raia 50 wa Korea Kaskazini ambao vibali vyao vya kukaa nchini humo vimepitwa na wakati licha ya marufuku ya kuzuia raia wa nchi hiyo kuondoka Malaysia.
Malaysia inasema kuwa watu hao walikuwa wakifanya kazi katika kisiwa cha Borneo.
- Korea Kaskazini ndiyo ilimuua Kim Jong-nam, yadai Korea Kusinii
- Mwili wa Kim Jong-nam walindwa vikali
Lakini haikusema ni kwa nini serikali imeamua kuwatimua, licha ya kuwepo marufuku ya kujibu hatua kama hiyo nchini Korea Kaskazini.
Uhusiano kati ya nchi hizo umesalia kuwa mbaya, tangu kuuawa kwa ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini nchini Malaysia mwezi uliopita.
Kim Jong-nam aliuawa kwa kemikali hatari kwenye uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur. Malaysia haijailaumu Korea Kaskazini moja kwa moja lakini kuna shaka kuwa Korea Kaskazni ilihusika.
Wachunguzi wamekwa wakiitaka Korea Kaskazini iwasalimishe washukiwa watatu kati yao wanaaminiwa kujificha ndani ya ubalozi wa Korea Kaskazia nchini Malaysia.
Lakini Korea Kaskazini imekuwa ikisisitiza kuwa Malaysia isalimishe mwili wa Kim Jong-nam na kukana vikali kumuua Kim.
Siku ya Jumatatu balozi wa Korea Kaskazini kwenye Umoja wa Mataifa, aliawambia waandishi wa habari kuwa kisa hicho ni njama mbaya kutoka kwa Marekani na Korea Kusini.
Marufuku hiyo ya usafiri imewaacha raia 9 wa Malyaia wakiwa wamekwam nchini Korea Kaskazini. Mamlaka nchini Malaysia nazo zinasema kuwa takriban raia 1000 wa Korea Kaskazini wamekwama nchini humo.
BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment