» » Baraza la wasichana lenye wanaume pekee laanzishwa Saudia

Baraza la wasichana lenye wanaume pekee laanzishwa Saudia


Baraza la wasichana lisilo na wasichana laanzishwa nchini saudiaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBaraza la wasichana lisilo na wasichana laanzishwa nchini saudia
Ni hatua nzuri kwa taifa linalojulikana kwa kutowapatia nafasi wanawake katika maisha ya umma.
Lakini wakati Saudia ilipotaka kuonyesha baraza lake la wasichana katika mkoa wa al-Qassim waliwaapuzilia mbali wanawake.
Picha zilizotolewa kuadhimisha baraza la kwanza la wasichana mkoani Qassim zilionyesha wanaume 13 jukwaani na hakukuwepo hata mwanamke mmoja.
Wanawake walikuwemo katika chumba chengine kupitia video.
Picha hizo za wanaume zimekuwa zikisambazwa katika mitandao ya kijamii baada ya mkutano huo kufanyika siku ya Jumamosi.
Imefananishwa na picha nyengine ya rais Donald Trump aliyezungukwa na wanaume akitia saini sera ya uavyaji mimba mnamo mwezi Januari.
Picha ya baraza hilo ni sawa na ile ya Trump alipotia saini sera ya uavyaji mimbaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionPicha ya baraza hilo ni sawa na ile ya Trump alipotia saini sera ya uavyaji mimba
Uzinduzi huo wa Saudia uliongozwa na mwanamfalme Faisal bin Mishal bin Saud, gavana wa mkoa huo aliyesema kuwa anafurahia mkutano huo ambao ni wa kwanza kufanyika katika ufalme huo.
''Katika mkoa wa Qassim tunawaangalia wanawake, akina dada zetu na wanaume na tunahisi tunajukumu kubwa la kuwafungulia fursa zitakazowahudumia wanawake na wasichana'', ,alisema.
Baraza hilo la wasichana liko chini ya uenyenkiti wa mwanamfalme Abir Bint Salman, na mkewe ambaye hakuwepo katika picha hiyo.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440


BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en


tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...