» » Magufuli: Hamuhitaji cheti cha kuzaliwa kufunga ndoa

Magufuli: Hamuhitaji cheti cha kuzaliwa kufunga ndoa

Haki miliki ya pichaIKULU YA DAR-ES SALAAMImage captionRais John Pombe Magufuli wa Tanzania

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amelifuta agizo lililotolewa waziri wa katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe linalowataka watu wote wanaotaka kufunga ndoa kuwa na cheti cha kuzaliwa kuanzia tarehe mosi mwezi Mei 2017.

Magufuli amefuta agizo wakati akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuondoka katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma na kurejea Jijini Dar es Salaam.

Je ndoa ni 'kupata jiko'? mchungaji azua zogo AbujaRoboti inayoweza kushiriki ngono kutengezwa

Kiongozi huyo amesema kuwa serikali haiwezi kuruhusu sharti hilo kutumika kwa kuwa litawanyima haki ya kuoa na kuolewa Watanzania wengi ambao hawana vyeti vya kuzaliwa, huku utaratibu wa kupata vyeti hivyo ukiwa bado unakabiliwa na changamoto nyingi kwa wanaohitaji.

Amesema hadi kufikia sasa idadi ya Watanzania walio na vyeti vya kuzaliwa ipo chini ya asilimia 20 huku wengi wao wakiwa ni wananchi wanaoishi vijijini ambako ni vigumu kupata vyeti hivyo, na wengine wakiwa ni waliozaliwa kabla ya kuanza kutolewa kwa vyeti vya kuzaliwa nchini mwaka 1961.

Eneo hatari zaidi la kufungia ndoa duniani?‘Mapenzi yetu yalizidi yote’Eneo hatari zaidi la kufungia ndoa duniani?

''Kwa hiyo ndugu zangu Watanzania msiwe na wasiwasi wowote, endeleeni na utaratibu wenu wa kuoa na kuolewa kama kawaida na kama kuna kifungu chochote cha sheria kinachomlazimisha mtu awe na cheti cha kuzaliwa ndipo aoe ama aolewe nitamuelekeza waziri wa katiba na sheria Mhe. Harrison Mwakyembe apeleke bungeni kikarekebishwe" amesema Magufuli.

Wakati huohuo Magufuli ametoa wito kwa wanasheria kuzikagua vyema sheria zinazohusiana na kuzaliwa na kifo na kuoa na kuolewa ili zisilete mkanganyiko kwa wananchi.

Waliokamatwa kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa waachiliwaPolisi watibua ndoa ya wapenzi wa jinsia moja Nigeria

Hata hivyo rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kupata vyeti vyao vya kuzaliwa kama kawaida na amewataka viongozi wote kuwahamasisha wananchi kuwa na vyeti hivyo.

Mada zinazohusiana

Tanzania

Mshirikishe mwenzako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles