Madaktari wamaliza mgomo nchini Kenya
Serikali ya Kenya pamoja na madaktari nchini humo, hatimaye wametia sahihi makubaliano ya kurudi kazini.
Hii ni baada ya mgomo wa madaktari nchini kenya, ambao umedumu siku mia moja na kuathiri vibaya huduma za afya nchini humo.
- Madaktari Kenya wakataa nyongeza ya serikali
- Hospitali zaanza kuwafuta kazi madaktari Kenya
- Hospitali za kibinafsi kujiunga kwenye mgomo Kenya
Chama cha madaktari kikiongozwa na mwenyekiri wake Oroko Samuel, kuliungana na waziri wa Afya Cleopha Mailu kwenye ofisi za magavana wakati wa kutiwa sahihi makubaliano hayo.
Makubaliano hayo yalitiwa sahihi mbele ya viongozi wa kidini.
Awali kulikuwa na hofu wakati madaktari walikataa kuingia ofisi ambapo makubaliano hayo yangetiwa sahihi, wakilalamikia utata wa vipengee fulani.
Madaktari walianza mgomo huo wakidai kuwa serikali imeshindwa kutimiza makubaliano waliyoafikiana, ya nyongeza ya mishahara yao na kuboreshwa kwa mazingira ya kufanya kazi.
Wiki iliyopita rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, alitangaza kuwa madaktari wangechukuliwa hatua iwapo hawangemaliza mgomo wao.
BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment