» » » Kathrada: Aliyepiga vita ubaguzi wa rangi Afrika Kusini afariki akiwa na miaka 87

Kathrada: Aliyepiga vita ubaguzi wa rangi Afrika Kusini afariki akiwa na miaka 87


Image captionKiongozi mwanaharakati aliyeshiriki sana kupigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Ahmed Kathrada amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87, wakfu wake umetangaza.
Bw Kathrada alifariki dunia akiwa katika hospitali moja mjini Johannesburg "baada ya kuugua kwa muda mfupi, kufuatia upasuaji aliofanyiwa kwenye ubongo wake".
Pamoja na Nelson Mandela, Bw Kathrada alikuwa miongoni mwa wanaharakati wanane wa African National Congress waliohukumiwa kufungwa jela maisha mwaka 1964.
Walipatikana na hatia ya kujaribu kupindua serikali ya ubaguzi wa rangi.
Bw Kathrada alikaa jela miaka 26, 18 kati ya miaka hiyo akiwa katika gereza hatari la Robben Island.
Aliachiliwa huru mwaka 1989.
Rais Mandela baadaye alimshawishi kujiunga na serikali.
Ahmed Kathrada aliondoka bungeni 1999, lakini aliendelea kushiriki katika siasa nchini humo.
Alikosoa mwelekeo wa chama cha ANC hivi majuzi na kumtaka Rais Jacob Zuma kujiuzulu.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...