» » Japan yaondoa wanajeshi wake Sudan Kusini

Japan yaondoa wanajeshi wake Sudan Kusini

Haki miliki ya pichaAFPImage captionJapan yaondoa wanajeshi wake Sudan Kusini

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe ametanza kuwa serikali ya Japan itaondoa wanajeshi wake kwenye kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini ifikapo mwishoni mwa mwezi Mei.

"Huku Sudan Kusini ikiingia kipindi kipya cha ujenzi wa taifa, tumeamu kusitisha jitihada za ujenzi ambao jeshi letu lilikuwa likitekeleza mjini Juba," bwana Abe alinukuliwa na shirika la hari la Kyodo.

Korea kaskazini yarusha makombora JapanTrump kuongeza bajeti ya jeshi kwa dola bilioni 54Watu wenye vipara washerehekea Japan

Katibu wa mawaziri Yoshihide Suga, baadaye alisisitiza kuwa kuondolewa huku hakutokani na sababu ya kuzorota kwa usalama maeneo wanajeshi hao walikuwa wakifanya kazi.

Wanajeshi hao wa Japan waliowasili nchini Sudan Kusini mwezi Novemba mwaka 2016, ndio wa kwanza katika kipindi cha karibu miaka 70 kutumwa nje ya nchi, wakiwa na agizo la kutumia nguvu ikiwa itahitajika.

Sudan kusini iliyojitenga kutoka Sudan mwaka 2011, imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 2013.

Mshirikishe mwenzako 

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...