» » Jaji akataa kutoa uamuzi wa kupinga marufuku ya usafiri US

Jaji akataa kutoa uamuzi wa kupinga marufuku ya usafiri US

Image captionMaandamano dhidi ya agizo la usafiri nchini Marekani

Jaji wa mahakama moja katika jimbo la Washington Marekani amekataa kutoa agizo la muda la kusitisha marufuku mpya ya usafiri iliyotolewa na rais Trump.

Jaji huyo, James Robart, amewataka mawakili wanaowakilisha majimbo yanayopinga marufuku hiyo kutoa ushahidi zaidi.

Wanasema amri mpya ya Trump dhidi ya raia wa mataifa 6 ya kiislamu si tofauti sana na marufuku ya awali ambayo jaji huyo alisitisha.

Marufuku hiyo inafaa kuanza kutekelezwa alhamis ijayo, japo inakabiliwa na vikwazo chungu nzima vya kisheria kutoka kwa majimbo kadhaa yanayosema marufuku hiyo inakiuka katiba.

Lakini jaji huyo alisema kuwa ana sababu za kutofanya hivyo.

Amesema kuwa lazima walalamishi wawasilishe ombi kabla ya yeye kutoa uamuzi wake.

Trump agonga mwamba Mahakama ya RufaaMahakama yakataa kurejesha marufuku ya TrumpMarekani: Idara ya haki yatetea marufuku ya TrumpDonald Trump asema atatoa marufuku mpya

Idara ya haki nchini humo ilikuwa imesema kuwa kwa sababu marufuku ya kwanza ya uhamiaji ilikuwa imepingwa na mahakama jaji huyo hangeweza kutoa uamuzi wa moja kwa moja.

Wale wanaopinga maraufuku wanasema kuwa ina athari sawa na ile ya hapo awali.Wamesemakuwa hatua hiyo ni kinyume na katiba na inaharibu biashara katika jimbo la Washington.

Msemaji wa Ikulu ya Whitehouse Sean Spicer amesema kuwa anaamini kuwa agizo hilo jipya litaidhinishwa na mahakama.

Majimbo kadhaa pia yamewasilisha maombi ya kupinga sheria hiyo.

Mshirikishe mwenzako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...