» » Ivanka Trump kuwa msaidizi wa babake Marekani

Ivanka Trump kuwa msaidizi wa babake Marekani

Haki miliki ya pichaEPAImage captionIvanka Trump (pili kulia) amesema alikuwa akifanya kazi kwa nia jema

Ivanka Trump amejiunga rasmi na serikali ya babake ambapo atahudumu kama mfanyakazi asiyelipwa, kwa mujibu wa ikulu ya White House.

Cheo chake halisi kitakuwa Msaidizi wa Rais.

Binti huyo wa rais wa Marekani amekubali shinikizo baada ya wataalamu kuhusu maadili kukosoa mpango wake wa awali wa kutaka kuhudumu katika wadhifa usio rasmi.

Bi Trump, 35, amesema amesikia "maswali ambayo baadhi ya watu wamekuwa wakiuliza kuhusu hatua yangu kumshauri rais katika nafasi yangu kama mtu binafsi".

Familia ya Donald Trump: Wake na watoto

Mumewe, Jared Kushner, ni mshauri mwandamizi wa Rais Donald Trump.

Kupitia taarifa, White House imesema ina furaha kwamba "Ivanka Trump amechukua hatua hii isiyotarajiwa katika nafasi yake kama binti wa rais".

Haki miliki ya pichaAFPImage captionIvanka Trump amekuwa akihudhuria mikutano ya Trump na viongozi wa dunia

Bi Trump alisema kupitia taarifa yake kwamba amekuwa akifanya kazi "kwa nia jema na kundi la washauri wa rais White House pamoja na mshauri wake binafsi kujadili kuhusu jukumu lake".

Wataalamu kuhusu maadili walilalamika ilipobainika wiki iliyopita kwamba Bi Trump angepewa afisi White House pamoja na kibali cha usalama cha kuingia na kuondoka ikulu hiyo, bila yeye kujiunga rasmi na wahudumu wa rais.

Mabinti wa marais wenye ushawishi kama baba zaoWatakaoumia na watakaofaidi chini ya Trump Marekani

Wakosoaji walisema kazi ya Bi Trump inafaa kufanywa rasmi ndipo aweze kudhibitiwa na sheria kuhusu uwazi wa maafisa wa serikali pamoja na maadili. Aidha, adhibitiwe na sheria kuhusu mgongano wa maslahi.

Wakili wa Bi Trump, Jamie Gorelick, amesema mteja wake atawasilisha nyaraka zifaazo za kufichua utajiri wake kwa mujibu wa sheria kuhusu maadili ya watumishi wa umma Marekani.

Haki miliki ya pichaEPAImage captionWiki mbili zilizopita, Bi Trump aliketi pamoja na Angela Merkel, kiongozi huyo wa Ujerumani alipokuwa ziarani Marekani

Mada zinazohusiana

SiasaDonald TrumpMarekaniWanawake

Mshirikishe mwenzako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles