» » Fedha za maendeleo zaongezeka kwa asilimia 36.......Tazama Hapa Ripoti Kamili Iliyowasilishwa Leo Bungeni na Waziri wa Fedha

Fedha za maendeleo zaongezeka kwa asilimia 36.......Tazama Hapa Ripoti Kamili Iliyowasilishwa Leo Bungeni na Waziri wa Fedha

Serikali imewasilisha mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa na kiwango cha ukomo wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18 huku ikionyesha ukomo wa bajeti kufikia shilingi trilioni 31.6 kutoka trilioni 22 za mwaka wa fedha unaoisha Juni 30, mwaka huu

Katika bajeti hiyo, fedha za maendeleo zimeongezeka kutoka trilioni 11.8 mwaka 2016/17 hadi trilioni 11.9 mwaka 2017/18 sawa asilimia 38 ya bajeti yote.

Mapendekezo hayo yamewasilishwa hii leo bungeni mjini Dodoma ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa vikao vya bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Akiwasilisha mapendekezo hayo, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango ametaja baadhi ya maeneo ya kipaumbele kuwa niujenzi wa reli ya kati, kuhuisha shirika la ndege Tanzania na shamba la kilimo na uzalishaji sukari la Mkulazi.

Aidha, Waziri Dkt. Mpango ametaja changamoto za utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/2017 hadi Februari mwaka huu kuwa ni mwamko mdogo wa kulipa kodi na hususani kuzingatia matumizi ya mashine ya kielektroniki.

Baadhi ya wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi, nje ya ukumbi wa bunge wamesema serikali imechukua jitihada kubwa katika kuhakikisha inaondokana na utegemezi kuliko kutegemea fedha kutoka nje.

Wabunge bado wanaendelea na vikao na shughuli za utekelezaji katika kamati mbalimbali hadi Aprili 2 mwaka huu kabla ya kuanza kwa vikao vya Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania April 4 mwaka huu mjini Dodoma.

==>Hii ndo Ripoti kamili iliyowasilishwa leo Bungeni


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440


BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en


tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles