» » Chumba cha kaburi alimozikwa Yesu chafunguliwa tena Israel

Chumba cha kaburi alimozikwa Yesu chafunguliwa tena Israel

Haki miliki ya pichaAFP/GETTY

Chumba kidogo kinachofunika kaburi ambako inaaminika Yesu Kristo alizikwa kimefunguliwa rasmi tena baada ya kufanyiwa ukarabati kwa miezi tisa.

Chumba hicho ambacho kinapatikana katika Kanisa la Kaburi la Yesu Kristo katika maeneo ya mji wa zamani wa Jerusalem kilikuwa kimekuwa dhaifu sana kiufundi.

Aidha, kilikuwa limebadilika rangi na kuwa karibu rangi nyeusi kutokana na masizi ya mishumaa mingi ambayo huwashwa eneo hilo.

Kanisa takatifu lafunguliwa IsraelMji wa kale sana wagunduliwa Misri

Mzozo kati ya madhehebu matatu ambayo kwa pamoja husimamia kanisa hilo - Kanisa la Kiothodoksi la Ugiriki, Kanisa la Kiarmenia na Kanisa Katoliki la Kirumi - ulichelewesha ukarabati huo kwa miongo mingi.

Antonia Moropoulou, aliyesimamia ukarabati, amesema chumba hicho sasa kimepata tena rangi yake asili inayokaribia hudhurungi.

Chumba hicho kilifanyiwa ukarabati mara ya mwisho mwaka 1810.

Mada zinazohusiana

IsraelDini

Mshirikishe mwenzako 

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...