Buhari: Sijawahi kuwa mgonjwa kupitia kiasi
Image captionRais Buhari aliwasili kutoka Uingereza kwa ziara rasmi ya kimatibabu
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema kuwa hajawahi kuwa mgonjwa kupita kiasi kama alivyokuwa katika majuma ya hivi karibuni.
Alikuwa akizungumza na maafisa wakuu mjini Abuja baada ya kurudi nyumba kufuatia likizo ya wiki saba ya kimatibabu nchini Uingereza.
Kutokuwepo kwake kulizua wasiwasi nchini Nigeria huku watu wakitoa uvumi kuhusu afya yake.
Je Aisha Buhari ni nani?Buhari kukaa muda zaidi UingerezaBuhari na Wasichana wa ChibokBuhari aongeza muda wa matibabu Uingereza
Makamu wa rais Yemi Osinbajo alichuku majukumu ya rais na msemaji wa rais amesema kuwa iongozi huyo atachukua mamlaka kuanzia siku ya Jumatatu.
Rais huyo mwenye umri wa miaka 74 aliwasili katika uwanja wa Kaduna kutoka Uingereza siku ya Ijumaa alfajiri.
Licha ya kuzungumza kuhusu alivyokuwa akijihisi, bwana Buhari hakutoa maelezo yoyote kuhusu hali yake.
Mshirikishe mwenzako
No comments:
Post a Comment