Kiangazi chahatarisha maisha nchini Kenya
Zaidi ya watu milioni 2 wameathirika kutokana na kiangazi kinachoendelea kukumba maeneo mengi nchini Kenya na kusababisha maafa kwa binadamu na mifugo.
- Mfugaji asimama kando ya mifupa ya mifugo wake waliofariki kutokana na kiangazi kinachoendelea katika kijiji cha Watiti, Moyale kaunti ya Marsabiti kaskazini mwa Kenya. Maelfu ya mifugo wamekufa kutokana na ukosefu wa maji na lishe
- Wafugaji wamzingira ngombe aliyekufa baada ya kuisha nguvu karibu na bwawa la maji lililobaki na maji katika eneo la Ambalo, Moyale, kaunti ya Marsabit.
- Zaidi ya watu milioni 2 wameathiriwa na kiangazi kutokana na ukosefu wa mvua tangu mwishoni mwa mwaka uliopita. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kiangazi kuwa janga la kitaifa na kuomba msaada wa kimataifa.
- Wanawake wengi wanakesha kwenye maeneo machache yaliyobaki na maji wakisubiri nafasi ya kuteka maji, na wanasafiri umbali mrefu kuelekea visimani na kurudi nyumbani.
- Zaidi ya 95% ya mabwawa ya maji yamekauka katika eneo Moyale kaunti ya Marsabit. Wafugaji wanasafiri umbali mrefu kutafuta maji, wengine wakivuka mpaka kuelekea Ethiopia kutafuta maji
- Katika kijiji cha watiti eneo la MOyale, wafugaji wanagawana chakula chao cha nyumbani na mifugo kutokana na ukosefu wa lishe. Mifugo wengi wamekufa kutokana na ukosefu wa chakula na maji, pamoja na kutembea umbali mrefu kutafuta maji na lishe.
- Mfanyikazi wa shirika la uhisani World Vision katika mojawepo wa bwawa lililokauka katika eneo la Moyale. Bwawa hili lilikuwa tegemeo la zaidi ya ffamilia mia tano na maelfu ya mifugo.
- Maelfu ya mifugo wanategemea mabwawa machache yaliyobaki na maji katika kaunti ya Marsabit na huenda mifugo hawa wakafa iwapo mvua inayotarajiwa kunyesha mwezi Aprili itakosa kunyesha.
- Mifugo ni kitega uchumi kwa jamii za wafugaji kaskazini mwa Kenya na zaidi ya 80% hutegemea kipato kutokana na mauzo ya mifugo. Kaunti ya Marsabit ina mifugo zaidi ya milioni 4.
- Mvua fupi zilizotarajiwa kunyuesha katika maeneo ya kasakzini mwa Kenya zilifeli na kusababisha kiangazi kikubwa kinachotishia kusababisha maafa nchini Kenya
- Kiangazi kimesambaratisha familia nyingi katika kaunti ya Marsabit ambapo watu wanahamahama wakitafuta maeneo yaliyo na maji na lishe, watoto wakiachwa na mababu.
- Inatabiriwa kwamba maelfu ya wanyama watakufa iwapo mvua itaendelea kuadimika katika kipindi cha wiki chache zijazo. Maisha ya binadam pia huenda yakaangamia katika kaunti ya Marsabit na kaunti zingine zilizo karibu kama vile Turkana.
- Mifugo wanaishi kwa maji pekee, kwani ardhi imegeuka vumbi. Elijah Chiwe anayesimamia shirika la uhisani la World Vision kaunti ya Marsabit, anasema hali huenda ikadorora iwapo wadau hawatachukua hatua ya kudumu ya kukabiliana na hali hii.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:
Post a Comment