» » Alichokisema Mkuu wa Majeshi Kuhusu Deni la Tanesco

Alichokisema Mkuu wa Majeshi Kuhusu Deni la Tanesco


Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Venance Mabeyo amesema Jeshi lake lipo tayari kupunguza deni linalodaiwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Bilioni 3, huku akiahidi kesho Jumatatu kuanza kwa kupunguza deni hilo.

Akizungumza na waandishi wa Habari Makao Makuu ya Jeshi (Ngome) Jijini Dar es Salaam amesema deni hilo limetokana na matumizi makubwa ya umeme, ukubwa wa jeshi lenyewe na mgawanyiko wake nchi nzima, zana wanazotumia huku nyingine zikilazimika kuwashwa muda wote kwa saa 24 kwa lengo la kulinda na kuimarisha ulinzi wa Taifa.

"Baada ya kupokea maelezo ya Tanesco na kufuatia tamko la Rais, Jeshi la Wananchi limetafakari na limefanya jitihada kupata fedha za kupunguza deni hili, tunadaiwa fedha kiasi kinachozidi kidogo Sh3 bilioni na Tanesco peke yake, tayari nimeagiza watendaji wetu watafute kiasi cha Sh 1 bilioni na wahakikishe kesho Marchi 27, cheki inawafikia Tanesco haraka ili huduma hiyo iendelee kutumiwa." Alisema Mabeyo

Pamoja na hayo Mkuu huyo amesema ufinyu wa bajeti umekuwa changamoto kubwa kwao katika kukabiri mahitaji makubwa katika jeshi hilo.

Kwa upande mwingine Mabeyo ameshauri na kusisitizia kwa Taasisi nyingine za Serikali kulipa deni ili kuongezea Tanesco uwezo wa kutoa huduma bora zaidi sekata za utumishi pamoja na kwa wananchi kwa ujumla ambao mpaka sasa wanashida ya umeme.

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440






BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en





tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...