» » USHINDI HATIMAYE- SOMO: SAULI MATATANI

USHINDI HATIMAYE- SAULI MATATANI
Picha ya Kirumba Seventh-day Adventist Church
MHUBIRI: Mchungaji David Mbaga
MAHALI: Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini Mwanza
Mafungu:1 Samwel 28:3-13; 1 Samwel 25:1;Mhubiri 9:5-6,10; 1Thesalonike 4:13-16; Mwanz 2:7
Wewe unapokutana na adui unakimbilia wapi?Sauli alipokuwa akiona maadui alitetemeka na kutafuta waganga na wachawi ili watengeneze mambo yake.Mambo yakiwa magumu subiri miguuni pa Yesu mpaka amekutendea jambo.
WALIO KUFA WANAJUA LOLOTE?
Biblia inasema kwamba wafu “hawajui lolote kamwe.” Pia, inasema kwamba wafu ‘hawajiwezi katika kifo.’ (Mhubiri 9:5).Neno la Mungu linaeleza hivi: “Mungu akamfanya mtu kutoka katika mavumbi ya nchi na kupuliza katika mianzi ya pua yake pumzi ya uhai, naye mtu akawa nafsi hai.”(Mwanzo 2:7).
Sisi ni viumbe tulioumbwa kutokana na mavumbi tunapokufa, mawazo yetu yanapotea. Lazaro alipofufuliwa hakusema chochote kuhusu hali yake alipokuwa mfu, kwa kuwa wafu hawajui lolote. Shetani ndiye anayeendeleza uwongo kwamba nafsi haiwezi kufa na inaweza kuwadhuru walio hai. Hata hivyo, watu wanaoiamini Biblia wanalindwa wasipotoshwe na uwongo kama huo. Wamekuja kujua ukweli wa kwamba Shetani anajaribu kuwadanganya watu waamini wafu wanaweza kuwasiliana na walio hai.(Zaburi 115:17,2Petro 2:4,Kumb la 18:10,11)
KUNA AINA MBILI KUU ZA UFUFUO:
i)Ufufuo wa kwanza au ufufuo wa uzima. Wote waliolala katika Bwana watafufuliwa kwanza. Kufumba na kufumbua miili yao itabadilishwa tena na kuungana na wale walio hai ambao nao miili yao itabadilishwa na kuwa ya utukufu, kisha wote kwa pamoja watakwenda kumlaki Bwana Yesu mawinguni.
ii) Ufufuo wa hukumu au ufufuo wa aibu ambao ni ufufuo wa watenda mabaya au wenye dhambi wote. Baada ya kufufuliwa watahudhuria wote mbele ya kiti cha enzi, kikubwa, cheupe cha hukumu. Yesu Kristo mhukumu wa haki atawaonyesha waziwazi matendo yao maovu.Biblia inasema katika Ufunuo 20:5,11-15). Pumzi ya Mungu ikitoka mwili unarudi mavumbini,hauna kazi tena.Ikiwa unadukuduku,ugomvi na mtu,uadui,chuki,makwazo ni vema mkamaliza naye akiwa hai usingoje akafa utakuwa umechelewa Yesu ndiye mafanikio ya kweli ni Mungu anayejali mpelekee shida zako zote yuko tayari kukupa msaada HATIMAYE USHINDI.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...