» » USHINDI HATIMAYE- SOMO: NAMNA YA KUREJESHA (1)

USHINDI HATIMAYE- NAMNA YA KUREJESHA (1)
Mhubiri: Mchungaji David Mbaga

Mhali: Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini Mwanza katika mahubiri yaliyo dhaminiwa na chama cha wanataaluma na wajasiriamali(ATAPE)
Mafungu: 1 Samwel 29:10-11;1 Samwel 30-1-8;Yoh 10:10; Kumbuk 31:20

…“Nakutakia afya njema ya mwili kama ulivyo nayo rohoni”. (3 Yohana 3:2)

Ni vitu gani katika maisha yako ambavyo umevipoteza na unatamani kuvirejesha au kuvisalimisha kwa Bwana? Ni vitu gani shetani ameviiba kwako na sasa umepata ujasiri wa kuvirejesha ili Bwana atukuzwe?

Afya zetu ni karama ya thamani.Lishe inao mchango mhimu katika afya.Hivyo twapaswa kuonesha nidhamu jinsi gani na kujitawala pale tunapojaribiwa kula kile tujuacho siyo chema kwa afya zetu.Mungu alitupatia Kweli kwaajili ya manufaa yetu.Tunapopuuzia,tunajiletea madhara,na mara nyingi hivi ndivyo imetokea na wengi leo hii huugua.

Kile tulacho hutusaidia kutufanya tuwe vile tulivyo.Damu,mifupa,mafuta na nyama zetu zote hulishwa na chakula tulacho.Yeyote aliyewahi kuugua kwasababu ya kula kupita kiasi,au kula kitu kisichopasa,anajua vyema jinsi chakula kilivyo na mchango mkuu katika afya zetu,kimwili na pia kiakili.Hivyo basi,chakula ama ulaji wetu unao mchango katika mawazo yetu,jambo ambalo siyo la kushangaza kwani ubongo ndio makao makuu ya mawazo, na ubongo wetu huathiriwa na chakula tulacho.

Sukari ni ya kuepukwa,siyo tu kwa watu wanene,bali hata kwa watu wengine wenya kujali afya zao.Inahusika kwa kiasi kikubwa na tatizo la kuongezeka kwa unene wa kupindukia. Matumizi ya chumvi kupita kiasi ni kichocheo cha magonjwa ya moyo na shinikizo la damu yanayochangia vifo vingi vya watu duniani hivi sasa.

Soda pia imebainika kutokuwa na lishe ya aina yoyote zaidi ya maji na sukari . Matumizi ya soda na vyakula vya kemikali vinahatarisha maisha yetu na kuchangia kuharibu hali zetu kiroho. Kinywaji hiki kinahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa watoto na watu wazima, yakiwemo matatizo ya kuongezeka unene kupita kiasi, kisukari,ugonjwa wa moyo,ugonjwa wa ini na mengineyo. kinywaji aina ya soda ni hatari kwa binadamu, sawa na mtu anayevuta sigara au mtumiaji wa kinywaji aina ya kahawa.

Ukiwa na Yesu una uhakika wa afya njema maana atakufundisha namna bora ya kuutunza mwili katika afya njema.Ili kujua chakula bora yatupasa kujifunza mpango wa awali wa Mungu kwa lishe ya mwanadamu.Nafaka,matunda,kokwa na mbogamboga zilizoandaliwa kwa namna rahisi na yakawaida kadiri inavyowezekana ndiyo lishe bora ineemeshayo afya.Hutupatia nguvu,uwezo wa kustahimili, na uhodari kiakili na kiroho.TUKITUNZA AFYA YA MIILI YETU KATIKA YESU USHINDI NI HAKIKA.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...