» » Silaha za nyuklia: Marekani yaionya Korea Kaskazini

Silaha za nyuklia: Marekani yaionya Korea Kaskazini

Waziri wa ulinzi nchini Marekani James Mattis na mwenzake wa Korea Kusini Han Min-kooHaki miliki ya pichaAP
Image captionWaziri wa ulinzi nchini Marekani James Mattis na mwenzake wa Korea Kusini Han Min-koo
Waziri wa ulinzi nchini Marekani James Mattis amesema kuwa Korea Kaskazini itakabiliwa vikali iwapo itafanya utumizi wowote wa silaha za kinyuklia .
Bw Mattis yuko nchini Korea Kusini ambapo ameihakikisha Seoul Korea kwamba inaungwa mkono na Marekani.
Majaribio ya mara kwa mara ya makombora ya nyuklia yanayofanywa na Korea Kaskazini mbali na taarifa za uchokozi yanaendelea kutia wasiwasi mbali na kuyakasirisha mataifa ya eneo hilo.
Marekani ina wanajeshi wengi nchini Korea Kusini na Japan ikiwa ni mpango wa ulinzi wa baada ya vita.
Wanajeshi wa Korea Kusini na wenzao wa Marekani wakishiriki katika mazoezi ya pamojaHaki miliki ya pichaAP
Image captionWanajeshi wa Korea Kusini na wenzao wa Marekani wakishiriki katika mazoezi ya pamoja
Rais Donald Trump awali amenukuliwa akisema kuwa mataifa hayo mawili yanafaa kuilipa Marekani zaidi ili wanajeshi wake kusalia kukaa nchini humo.
Bw Mattis ametumia ziara yake nchini Korea Kusini kulihakikishia taifa hilo kwamba utawala wa bw Trump utaendelea kulinda eneo hilo.
Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa WHATSAP (+255) 0769436440 Karibu Sana Read More

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...