» » IBADA YA SABATO YA TAREHE 04/02/2017 SABATO YA KWANZA YA MWEZI FEBRUARI Kutoka Katika Kanisa La Waadventista Wasabato Udom- Mashariki (UDOM-EAST)._


IBADA YA SABATO YA TAREHE 04/02/2017

SABATO YA KWANZA YA MWEZI FEBRUARI

_Kutoka Katika Kanisa La Waadventista Wasabato Udom- Mashariki (UDOM-EAST)._
Image result for MBINGUNI

*SOMO:* ```USIKU WA MANANE```
*F/KUU:* _KUTOKA 12:42_
*WIMBO:* ~Na; 100 {Mlango Wazi}.~
*Na:* Rev; YASINI SAHANI.
   ✏ *KUTOKA 12:42*
Usiku wa pekee ambao Bwana aliutumia kuwakomboa waisrael kutoka utumwani misri.
  ✏ *MATHAYO 25:6*
Pakawa na kelele usiku wa manane Bwana harusi alipofika nao walitakiwa kumlaki.
➡ Wayahudi waliugawa usiku katika nyakati (zamu) nne. Na *USIKU WA MANANE* ulikuwa zamu ya Tatu.
Usiku huu kwa Wakati mwingine hutamkwa kama *saa ya ukombozi*
✏ *ISAYA 60:2*
Isaya anautamkaje Usiku?
Guza litaifunika dunia, giza kuu litazifunika kabila za watu. Lakini tumaini ni kuwa Bwana atakuzukia ww na nuru itaonekana.
✏ *Amosi 8:11*
Siku zinakuja ambazo Bwana ataleta njaa, si njaa ya kawaida ya hitaji la kula bali ni njaa ya kukosa kuyasikia maneno ya Bwana. Saa ya ukombozi yaja ambapo ulimwengu utakuwa katika giza kuu.
Hata wakati wa Yesu kulikuwa na giza kuu.
 Sifa za siku za mwisho zinazoashiria giza kuu;
~1: Matumaini ya watu wengi yatakuwa yamejengwa katika ulimwengu unaoangamia~ *(Mathayo 24:1)*
✏ *Isaya 24:19,20*
Dunia hii inaharibika sana, inavunjika, unapasuka, inatikisika, inalewalewa, inawayawaya, na mzigo wa dhambi zake unailemea na Mwisho itaanguka wala haitainuka tena. *HAKUNA TUMAINI KATIKA ULIMWENGU HUU*
▶ JE TUPATE WAPI TAARIFA SAHIHI ZA UANGAMIVU WA ULIMWENGU?
✒ *MATHAYO 24:37,28*
✏ *Kutoka 12:29.*
Kwa wengine itakuwa saa ya ukombozi lakini kwa wengine itakuwa saa Maangamizi kwa watu wengine.
Hakuna Maangamizi
yaliyofanyika bila maonyo.
     Wakati wa Nuhu.
     Wakati wa Luthu.
     Wakati wa Ninawi.
     Wakati wa Yohana Mbatizaji.
✏ *Mathayo 24:14*
Baada ya maonyo kusambaa ulimwenguni kote ndipo *usiku wa manane* utakuja, kwa maana Bwana hakufanya lolote bila maonyo.
✏ *Ufunuo 14:6*
Onyo latolewa juu ya ulimwengu wote, na malaika mwenyewe ataruka juu ya ulimwengu wote akisema *_Mcheni Mungu na Kumtukuza, Kwa Maana Saa ya Hukumu Iake Imekuja_*
✒ Saa ya kufanya maamuzi ndiyo sasa, maamuzi yako yatakufanya usimame sehemu salama au sehemu isiyo salama.
✒ Usiku wa manane mahali pengine hutafsiriwa kama *GIZA LA KIROHO*
> Ibada za mazoea kwa wengi.
> Kuutumainia ulimwengu kwa wengi.
> Maandalizi ya ujio wa Yesu yamepungua watu wanajishughulisha na shughuli za kidunia sana.
Na ndio kuja kwake mwana wa adamu kutakuwa kwa Kushtukiza kwa wengi, maneno ya Bwana yatawekwa katika nadharia na sio katika utendaji.
✒ Kurudi kwake Bwana ni hakika, na kila mmoja anatakiwa kufanya maandalizi kabla ya usiku kuujia ulimwengu. Nasi imetupasa kuuangazia ulimwengu wote kwa kuwa tu Nuru ya ulimwengu wote kabla ya giza kuu kuujia ulimwengu.
✒ Uzuri wa dunia ni kidogo sana, lakini kwa Baba yetu wa Mbinguni pana uzuri wa kutosha na jicho halijaona *Anasa Halisi* kama iliyo kwa Bwana.
Bwana akubariki unapofanya Mabadiliko katika kuutafuta wokovu.

Prepared by:
   *Pr: SABUYA_JR98.*
Watspp: +255 766 060 303
Facbook: Sabuya Willy Jr
Instagrm: Sabuya_Jr98

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...