» » Zaidi ya watu milioni moja wasaini barua kumzuia Trump kuzuru Uingereza

Zaidi ya watu milioni moja wasaini barua kumzuia Trump kuzuru Uingereza


Waziri Mkuu Teresa May alitangaza muwaliko huo wakati akiwa ziarani Marekani.Haki miliki ya pichaPA
Image captionWaziri Mkuu Teresa May alitangaza muwaliko huo wakati akiwa ziarani Marekani.
Zaidi ya watu milioni moja wa Uingereza wamesaini barua ya kutoa shinikizo kwa serikali ya Uingereza kusitisha ziara rasmi iliopangwa baadaye mwaka huu ya rais Donald Trump.
Barua hiyo iliyoandikwa kufuatia agizo la rais Trump dhidi ya wahamiaji, inaeleza kuwa kuja kwake kutamuaibisha Malkia Elizabeth.
Idadi ya watu wanaoendelea kusaini kupinga Mwaliko wa Trump nchini Uingereza inaendelea kuongezeka, tangu Marekani kuweka vikwazo dhidi ya wageni hatua iliyozua ghadhabu kote duniani. Amri ya Trump: Ni nani anaathirika?
Waziri Mkuu Teresa May alitangaza muwaliko huo wakati akiwa ziarani Marekani.
Afisi yake imesema japo haikubaliani na baadhi ya sera za Trump hata hivyo ni vyema Uingereza kuwa na ushirikiano wa karibu na Marekani.
Kiongozi wa Upinzani Jeremy Corbyin ametaka Waziri Mkuu kuahirisha ziara hiyo.
Maandamano zaidi kumpiga Trump yanatarajiwaHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionMaandamano zaidi kumpiga Trump yanatarajiwa
Wengi wanaopinga wanasema ziara ya Trump nchini Uingereza itakua aibu kwa Ufalme.
Ziara rasmi za serikali Uingereza huambatana na mualiko kutoka kwa Malikia, ambae huwapokea viongozi wawili wa nchi kila mwaka.
Aiki jana Rais Trump aliweka sheria kusitisha mpango wa kuwapokea wakimbizi na hasa kuwapiga marufuku wakimbizi wote kutoka Syria na wengine kutoka nchi saba zote zikiwa za kiisilamu.
Siyo mara ya kwanza kumekua na kampeini kumpiga Trump Uingereza.
Mwaka wa 2015 raia laki tano walisaini kutaka kiongozi huyo kupigwa marufuku Uingereza.
Kiongozi wa zamani wa chama cha Labour Ed Millibard amesema yeye na mbunge mwenzake ambae ni mzaliwa na Iraq Nadhim Zahawi wataitisha muswada wa dharura bungeni kujadili maombi ya raia.
Alex Salmond ambe alikua kiongozi wa Scotland amesema Trump hafai kupata muwaliko Uingereza, kauli yake ikiungwa mkono na Meya wa jiji la London Sadiq Khan
Teresa MayHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTeresa May
Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa WHATSAP (+255) 0769436440 Karibu Sana Read More

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...