» » Moussa Faki wa Chad ndiye mwenyekiti mpya wa tume ya AU

Moussa Faki wa Chad ndiye mwenyekiti mpya wa tume ya AU


Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Chad Moussa FakiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWaziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Chad Moussa Faki

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Chad Moussa Faki amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa tume ya Muungano wa Afrika AU.
Faki anachukua mahala pake Dlamini Zuma kutoka Afrika Kusini ambaye kipindi chake cha kuhudumu kimekamilika.
Mshindani ,mkuu wa bwana Faki katika duru ya mwisho ya upigaji kura, wakati wa kikao cha AU mjiji Addis Ababa, Ethiopia, alikuwa ni waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Kenya Amina Mohamed.
Wagombea watano waliokuwa wakiwania wadhifa huo ni pamoja na waziri wa mambo ya nchi za kigeni wa Kenya Amina Mohammed, mwanadiplomasia Abdoulaye Bathily kutoka Senegal, waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Chad Moussa Faki Mahamat, mwanasiasa mkongwe kutoka Botswanda Pelonomi Venson-Moitoi na aliyekuwa wakati mmoja mshauri wa rais wa Equatorial Guinea Mba Mokuy.
Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa WHATSAP (+255) 0769436440 Karibu Sana Read More

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles