» » Yanga washikilia tiketi ya Azam FC nusu fainali Mapinduzi Cup..

Yanga washikilia tiketi ya Azam FC nusu fainali Mapinduzi Cup..

Mabingwa wa soka Afrika Mashariki Azam FC ya Tanzania Bara italazimika kuifunga Yanga ili kufika nusu fainali ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kutoka suluhu na Jamhuri juzi.

Azam FC ilijikuta ikiambulia pointi moja baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Jamhuri ya Pemba katika moja ya mechi za mashindano hayo kwenye Uwanja wa Amaan hapa.

Wakati Azam wakisubiri `huruma’ ya Yanga, mabingwa hao wa Tanzania Bara (Yanga), wenyewe tayari wameshakata tiketi ya kucheza nusu fainali baada ya juzi kuifunga Zima Moto kwa mabao 2-0.

Kimsimamo, Yanga wana pointi sita baada ya kushinda mechi mbili wakati Azam wenyewe mkononi wanashikilia jumla ya pointi mbili.



Nahodha wa Azam FC, John Bocco alisema baada ya mchezo huo dhidi ya Jamhuri kuwa, Yanga ni timu kubwa na wana kazi ngumu watakapokutana nao kesho kwenye Uwanja wa Amaan.

“Tunawaheshimu Yanga kwa kuwa ni timu kubwa. Tunajua nasi ni timu kubwa na bora, itakuwa mechi ngumu sana. “Lakini tunaiweka kando mechi ya leo na tunaanza maandalizi kwa ajili ya mechi ijayo kujiandaa dhidi ya Yanga,” alisema.

Jamhuri ilichapwa mabao 6-0 na Yanga, hivyo kuondoka na pointi moja mbele ya Azam hakuna shaka kuwa matokeo hayo yatakuwa ni faraja kubwa sana kwao.

Pambano hilo la Yanga na Azam FC litafanyika kwenye Uwanja wa Amaan kuanzia 2:30 usiku.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...