» » Wamasai kuzuiwa kutembea na sime

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba anakusudia kupeleka bungeni muswada wa dharura ili kutunga sheria ya kupiga marufuku baadhi ya jamii na makabila kutembea na silaha.



Waziri Nchemba amekuja na wazo hilo kutokana na kuzuka upya kwa mapigano kati ya wakulima na wafugaji mkoani Morogoro, ambapo mbali na wakulima kukatwa na silaha zenye makali, Augustino Mtitu alichomwa mkuki mdomoni na kutokea shingoni wiki moja iliyopita.

Kabila la kifugaji la Wamasai, kwa mfano, hutembea na sime na fimbo, na ni jadi kwa jamii kadhaa za watunza mifugo wengine kubeba mikuki na mapanga.

Akizungumza na wanavijiji wa kata ya Tindiga, Kilosa mkoani Morogoro jana katika ziara yake ya siku mbili, Nchemba alisema serikali haitowavumilia watu wanaojichukulia sheria mkononi kwa kuwachoma watu mikuki, sime na mapanga, hususan katika maeneo yenye migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Waziri Nchemba alisema endapo matukio hayo yataendelea, serikali itawasilisha muswada wa dharura bungeni kuwa na sheria ya kuzuia baadhi ya makabila kutembea na silaha za kimila.

“Tunaanza kuhesabu matukio yanayohusu vitendo vya kinyama. Tukisikia tukio la kuchomwa mkuki, sime, mshale, kukatwa panga na kujeruhiwa na rungu au fimbo, tutapendekeza iwepo sheria kupiga marufuku watu kutembea na silaha ili atakayeonekana na silaha achukuwe hatua kali,” alisema.

UMWAGAJI WA DAMU
Nchemba alisema hakuna mazao, ng'ombe wala mbuzi mwenye thamani kuliko maisha ya binadamu.

Aidha alisema serikali kamwe haiwezi kuruhusu ardhi yenye rutuba imwagikiwe damu kutokana na vitendo vya kinyama wanavyofanyiwa binadamu.

“Kitendo cha umwagaji wa damu ni laana na serikali hatutakubali ardhi ya Morogoro yenye rutuba kugeuka laana kutokana na kumwaga damu ya watu wasiokuwa na hatia,” alisema.

Alisema tukio la Mtitu kuchomwa mkuki ni baya na aliyefanya hivyo alikuwa na nia ya kuondoa uhai wa mkulima huyo na kwa kuwa ameshafikishwa katika vyombo vya sheria, anatumaini sheria itachukua mkondo wake.

Katika hatua nyingine, Nchemba aliwaonya baadhi ya askari na watumishi wa serikali, ambao wanashirikiana na wafugaji wanaojiusisha na mauaji ya wakulima kuwa endapo watabainika wataunganishwa katika kundi la wahalifu wanaochochea umwagaji wa damu.

Aliwataka wakulima na wafugaji kufungua ukurasa mpya na kukemea vitendo hivyo.

Nchemba pia aliziomba jamii hizo kutaja wahusika serikalini ili wachukuliwe hatua.

Awali, wakulima walimwomba Waziri Nchemba wafugaji wanaoingiza mifugo katika mashamba yao kuchukuliwa hatua.

Salum Ally alisema kuwa kata ya Tindiga sasa inakabiliwa na upungufu wa chakula kutokana na mazao yaliyolimwa wakati wa mvua za vuli kuliwa na mifugo. Alisema wanahitaji chakula cha msaada.

Naye mmoja wa wafugaji kutoka Kijiji cha Malangali ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, alimwomba Waziri Nchemba kuwanusuru na migogoro hiyo kwa kuwasaidia kuwapa maeneo ya iliyokuwa ranchi na mashamba makubwa yanayohodhiwa na matajiri ili wafugie huko.

Alisema hawapendi wala kufurahishwa na migogoro hiyo, lakini wako baadhi ya wamiliki wa mashamba makubwa walioshindwa kuyalima, wanawakodisha wafugaji na kujikuta wanaingiza mifugo katika mashamba ya wakulima.
 
chanzo:  Nipashe

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...