» » RAISI Magufuli ahudhuria mkutano wa AU

Magufuli ahudhuria mkutano wa AU


Dr John MagufuliHaki miliki ya pichaAFP
Image captionDr John Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli, yuko mjini Addis Ababa nchini Ethiopia ambako anahudhuria mkutano wa 28 wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuia ya Umoja wa Afrika (AU).
Hii ndiyo mara ya kwanza ya Rais Magufuli anahudhuria mkutano huo tangu aingie madaraka kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba mwaka 2015.
Akiwa Addis Ababa Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Bara la Afrika wanaohudhuria mkutano huo, mkutano ambao pia utahudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
Mkutano huo pia utatumiwa kumchagua mwenyekiti mpya wa tume ya Umoja wa Afrika (AU).
Wale wanaowania wadhifa huo wa mwenyekiti ni pamoja na waziri wa mambo ya nchi za kigeni wa Kenya Amina Mohammed, mwanadiplomasia Abdoulaye Bathily kutoka Senegal, waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Chad Moussa Faki Mahamat, mwanasiasa mkongwe kutoka Botswanda Pelonomi Venson-Moitoi na aliyekuwa wakati mmoja mshauri wa rais wa Equatorial Guinea Mba Mokuy.

Wawania wa mwenyekiti mpya wa tume ya Umoja wa Afrika (AU).Haki miliki ya pichaAU
Image captionWawania wa mwenyekiti mpya wa tume ya Umoja wa Afrika (AU).
Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa WHATSAP (+255) 0769436440 Karibu Sana Read More

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles