» » Wanajeshi wa Kenya kurudi Sudan Kusini

Wanajeshi wa Kenya kurudi Sudan Kusini


Wanajeshi wa Kenya kurudi Sudan KusiniHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWanajeshi wa Kenya kurudi Sudan Kusini
Wanajeshi wa Kenya watajiunga tena na Ujumbe wa kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa baada ya kujiondoa mwaka jana kutokana na utata.
Taarifa kutoka Ikulu ya Rais wa Kenya imesema kuwa Umoja wa mataifa pia umekubali kuikabidhi tena Kenya uongozi wa majeshi hao.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guteress walikutana mjini Addis Ababa, Ethiopia ambapo kongamano la Umoja wa Muungano wa Afrika AU linaendelea.
Kulingana na taarifa yake Msemaji wa rais Manoah Esipisu, wawili hAo walikubaliana kurejesha uhusiano mwema ulioko kabla ya Kenya kujiondoa mwezi Novemba mwaka jana.
Umoja wa mataifa ulimtimua Kamanda wa Ujumbe, Luteni Jenerali Johnson Mogoa Ondieki aliye Mkenya, kufuatia ripoti kwamba wanajeshi wa umoja wa mataifa walichelea kuingilia kati huku raia na wafanyikazi wa misaada wakishambuliwa mjini Juba, Sudan Kusini.
Kenya ilisema uamuzi huo haukuwa wa haki na ikaamua kuondoa wanajeshi wake 1500 pamoja na kujiondoa kabisa kwenye shughuli za kutafuta amani nchini humo.
Bwana Guteress alisema amependekeza Kenya ichukue tena uongozi wa wanajeshi hao kama ishara ya imani kwa jeshi la Kenya. Maafisa wakuu wa Umoja wa mataifa na Kenya sasa wataanza majadiliano ya kukirejesha kikosi cha Kenya.
Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa WHATSAP (+255) 0769436440 Karibu Sana Read More

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...