Lukuvi awapania viongozi walevi wa madaraka
Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi hati 810 za kimila za kumiliki ardhi kwa wakazi wa Kijiji cha Kinywang’anga, Wilaya ya Iringa mkoani hapa.
“Tumejifunza kutokana na uzoefu tuliopata, migogoro mingi ya ardhi imetokana na baadhi ya viongozi wetu wa serikali za vijiji ambao wamekuwa wakibadilisha matumizi ya ardhi bila kufuata utaratibu,” alisema.
Lukuvi alisema Serikali haitasita kuwafuta kazi viongozi wa serikali za vijiji watakaobainika kujihusisha kubadili mpango wa matumizi bora ya ardhi za vijiji bila ya kushirikisha wananchi.
Alisema licha ya kuwaondoa kwenye nafasi zao, viongozi hao watakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID), Dan Thompson alisema wanaendesha miradi ya aina hiyo kwenye vijiji 41 vya mikoa ya Iringa na Mbeya kupitia Mradi wa Feed the Future.
Habari zaidi soma Gazeti la Mwananchi
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment