» » HILI ni jibu la Diamond kuhusu kwanini anataja majina ya wacheza soka kwenye ngoma zake.


Sio kitu cha ajabu kusikia wasanii wakiwarusha wanamichezo kwenye ngoma zao. Hiki kitu kimeanza muda mrefu sana ndani ya Africa hadi nje ya Africa. Mmoja kati ya wanamichezao waliohi kutajwa sana kwenye nyimbo za HipHop huko marekani ni Michael Jordan au M.J kama wanavyomuita.

Tumeongea na Diamond Platinumz ambapo yeye na wasanii wake wa WCB wamekua wakitaja majina ya wana michezo mara kadhaa kwenye ngoma zao hasa Ronaldo na Mbwana Samatta.

Diamond tulipomuuliza kuna faida gani kwake na kipi kinamvutia kutaja majina ya wachezaji hao kwenye ngoma zake. Jibu lilikua hili “Hata kama mtu anafanya kazi kiasi gani kama jamii haijamkubali basi bado ana kazi ya ziada ya kufanya hadi akubalike.”

Aliendelea “Sasa mimi nawataja watu ambao wamefanikiwa kukubalika na jamii, ukiangalia watu kama Ronaldo na Samatta inaongeza chachu ya nyimbo na kupendwa zaidi. Hata wao pia wanafarijika kuona kwamba sisi kwa sisi pia tunakubaliana kwa kila kitu tunachofanya.”

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...