» » CCM Malinyi kuwalinda wenye kasi ya maendeleo

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya za Ulanga na Malinyi, kimeonya tabia ya baadhi ya watendaji serikalini kuwaonea wivu watendaji wenzao wanaosimamia na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho kwa kasi na nguvu, na kimeahidi kuwalinda viongozi wenye kasi ya maendeleo kwa nguvu zote.
Hayo yalisemwa na Katibu wa CCM wa Wilaya za Ulanga na Malinyi, Jasmin Kihele, alipokuwa akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya CCM katika wilaya hizo muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo na Katibu Tawala (DAS) mpya wa Wilaya ya Malinyi, Lameck Lusesa aliyefika ofisini kwake kujitambulisha ambapo pia alikabidhiwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa ajili ya utekelezaji.
Kihele alisema kutokana na Falsafa ya Hapa Kazi Tu iliyoasisiwa na Rais John Magufuli, wapo watendaji katika Wilaya za Ulanga na Malinyi wamekuwa mfano wa kuigwa katika uchapaji wa kazi kwa vitendo, lakini wameanza kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa watendaji wenzao ambao kwa makusudi wameamua kuanza kuwakwamisha kutokana na kuwaonea wivu jambo alilosema halikubaliki.
“Niseme wazi kuwa hatutakubali. Kwa bahati nzuri Kamati ya Siasa ya Wilaya haipokei taarifa ikiwa ofisini, inakwenda kukagua utekelezaji wa miradi na tunaona kwa macho yetu ni viongozi gani wanafanya kazi nzuri. Hawa tutawapigania kwa nguvu zetu zote, maana serikali ya sasa si ya ujanja ujanja ni ya wachapa kazi,” alisema.
Alisema hali ya kisiasa katika Wilaya za Ulanga na Malinyi ni nzuri kutokana na wakurugenzi wake wakishirikiana na watendaji wengine kufanya kazi kwa bidii usiku na mchana hatua inayoharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kupunguza kero za wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, uchumi, miundombinu na kero za kijamii.
“Tumefika Malinyi, kwa kweli kazi inafanyika kwa kiwango cha kuridhisha. Viongozi wa Malinyi wakiongozwa na Mkurugenzi wake (Marcelin Ndimbwa) wanafanya kazi. Utendaji huu umefanya hali ya kisiasa kuwa nzuri sana maana hata katika maeneo ambayo yalichukuliwa na upinzani, wameanza kutuunga mkono kutokana na kazi inayofanyika. Hawa ndio viongozi wa aina ya serikali ya awamu ya tano. “Na hata sisi si kwamba tunafika na kuangalia tu, yapo maeneo ambayo tunashirikiana na viongozi wakiwemo wakurugenzi kujenga miradi ya maendeleo kama ambavyo Katibu wetu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambavyo amekuwa anafanya,” alisema.
Akimkabidhi Ilani DAS Lusesa, Kihele alisema chama hicho kitapima utendaji wa DAS huyo kwa kuangalia utekelezaji wa Ilani na si kuangalia wingi wa majungu au maneno atakayoyasema, kwani lengo ni kuona serikali ya CCM inawatumikia wananchi na hasa wanyonge.
“Dira yetu ni Ilani na si maneno au majungu. Kuthibitishwa kwako na chama kunategemea usimamiaji na utekelezaji wa Ilani hii. Tunaomba ukafanye kazi kwa bidii ili kuharakisha maendeleo ya watu wa Malinyi,” alisema.
Kwa upande wake DAS Lusesa aliahidi kufanya kazi kwa bidii, akisema lengo ni kuhakikisha kuwa anafikia malengo ya chama na serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi na aliahidi kutoa msukumo na kushirikiana kwa karibu na viongozi na watendaji wa Malinyi katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa kasi na viwango.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...