» » Uteuzi: Mhandisi Boniface Gissima ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa REA

Bodi ya Nishati Vijijini (REB) imemteua Mhandisi Boniface Gissima NyamoHanga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala Dk.Lutengano Mwakahesya aliyestaafu mwezi Juni 2016.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini Dk.Gideon Kaunda inaeleza kuwa uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria namba 8 ya mwaka 2005 ya Nishati Vijijini katika kikao kilichofanyika Tarehe 17 Desemba 2016.

Aidha taarifa hiyo inaeleza kuwa kabla ya uteuzi huu Mhandisi Gissima Nyamo­Hanga alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Imeongeza kuwa Mhandisi Gissima ana uzoefu wa miaka 20 katika Sekta ya Nishati na pia ameshika nyadhifa mbalimbali tangu mwaka 2008 alipoajiriwa REA.

Mbali na hayo Mhandisi huyu amehitimu Shahada ya Uhandisi katika fani ya Umeme, Shahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Uhandisi,Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara (MBA) zote kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Stashahada ya Juu ya Sheria na Upatanishi na Usuluhishi ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Dar es Salaam.

Bodi ya Wakala wa Nishati ya Umeme Vijijini (REA) inaomba sekta mbalimbali kumpatia ushirikiano Mhandisi Boniface Gissima Nyamo­Hanga ili kumuwezesha kutekeleza majukumu na malengo yake.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...