John Glenn, Mmarekani wa kwanza kuizunguka dunia afariki
Mwana anga wa zamani John Glenn, ambaye alikuwa Mmarekani wa kwanza kuizunguka dunia kupitia mzingo wa dunia, amefariki dunia akiwa na miaka 95.
Alikuwa mwanajeshi wa zamani na alihudumu pia kama seneta.
Glenn alikuwa amelazwa hospitalini Columbus, Ohio, kwa zaidi ya wiki moja na alifariki akwia amezingirwa na wanawe na mke wa miaka 73.
Glenn anafahamika sana kwa kuizunguka dunia mwaka 1962 akiwa na chombo cha anga za juu cha Friendship 7.
Ufanisi wake uliashiria wakati ambao Marekani iliufikia Muungano wa Usovieti katika kutumma binadamu anga za juu.
Glenn atazikwa katika makaburi ya Arlington, Virginia.
Aliporejea duniani, Glenn alichaguliwa seneta wa chama cha Democratic mwaka 1974, ambapo alihudumu kwa miaka 24.
Mwaka 1998, miaka 36 baada ya safari yake ya kihistoria anga za juu, aliandika historia tena kwa kuwa mtu mzee zaidi kwenda anga za juu, akiwa na miaka 77.
Glenn alizaliwa 1921 Cambridge, Ohio.
Rais Barack Obama ameongoza Wamarekani kutoa heshima zao kwa Glenn, ambapo amemtaja kama "rafiki aliyetutoka".
Aliwania kuwa mgombea urais mwaka 1984, lakini akashindwa na Walter Mondale.
Glen alitunukiwa tuzo ya dhahabu kwa Kiingereza, Congressional Gold Medal, tuzo ya juu zaidi inayopewa rais Marekani mwaka 2011.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment