» »Unlabelled » Trump aondoshwa jukwaani na maafisa wa usalama

Trump aondoshwa jukwaani na maafisa wa usalama

  • 6 Novemba 2016
Mshirikishe mwenzako
Mgombea wa urais nchini Marekani Donald Trump akiondoshwa katika jukwaa na maafisa wa usalama
Image captionMgombea wa urais nchini Marekani Donald Trump akiondoshwa katika jukwaa na maafisa wa usalama
Mgombea wa urais wa Marekani kwa tikiti ya chama cha Republican Donald Trump ameimarisha kampeini zake mjini Nevada licha ya kisa cha usalama kilochobabisha walinzi wake kumuondoa jukwaani kwa muda.
Wafuasi wake wanasema walinzi wake walifanikiwa kumuondoa jukwaani licha ya hofu kwamba kulikuwa na mtu aliyekuwa amejihami kwa silaha miongoni mwao.
Bw.Trump alikuwa anakaribia kilele cha hotuba yake ndani ya ukumbi wa Reno uliyojaa wafuasi wake, na ghafla kukatokea rabsha karibu na jukwaa.
Taharuki ilitanda mahala hapo kabla ya walinzi wake kufanikiwa kumuondoa.
Wafuasi wake waliyojawa na hofu walianza kukimbilia lango la kutoka nje wa ukumbi huo kufuatia madai ambayo hayakudhibitishwa
Polisi wamemkamata mtu mmoja kufuatia tukio hilo lakini akaachiliwa muda mfupi baadaye.
Mtu huyo hakupatikana na silaha kama ilivyodaiwa.
Huku zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya uchaguzi mkuu,wagombea wote wawili wameimarisha kampeini zao katika jimbo muhimu la Florida linalo na umaarufu wa kuamua mshindi wa uchaguzi wa urais.
Kumekuwa na ongezeko la watu wa asili ya hispania wanaopiga kura mapema Florida na Nevada.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema huenda hatua hiyo ikamnufaisha Bi Clinton.
Trump amesema atazuru jimbo la Minnesota ambalo chama cha Republican hakijawahi kupata ushindi kwa zaidi ya miaka arobaini.
Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa au tupigie kwa (+255) 0769436440 Karibu Tena

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...