Mtu na Mwumbaji Wake
Elifazi asingeweza kushinda kabisa tuzo yo yote ya hekima na huruma, kwa maneno yake ya ufunguzi. Kimsingi alikuwa anasema kwamba ilikuwa ni rahisi kwa Ayubu kuwa nuru na faraja kwa watu wengine mambo yalipokuwa yanakwenda vizuri. Lakini sasa kwa sababu mabaya yamemkuta, “anapata tabu.” Na wala, hakutakiwa kujisikia hivyo. Mungu ni mwaminifu, na kwa hiyo mabaya huja kwetu pale tunapostahili kuyapata.
“Soma Soma Ayubu 12:21. Elifazi anatoa hoja gani nyingine kwa Ayubu?
Kuna mambo mengi ya kushangaza ambayo mtu anaweza kuyaangalia hapa, ikiwemo namna hawa watu walivyoielewa hulka na tabia ya Mungu wa kweli, hata kabla ya kuwepo kwa taifa la Israeli. Kitabu hiki kinatuonesha kwamba, bila shaka kulikuwa na watu wengine waliokuwa wanajua habari za Mungu wa kweli, hata kabla ya wazee na hatimaye Waisraeli. Kwa upande mwingine, hapa, tunamwona Elifazi akijaribu kuitetea tabia ya Mungu.
Kile alichokisikia Elifazi katika “maono ya usiku” kilikuwa teolojia sahihi kwa namna nyingi (angalia Zaburi 103:14;Isaya 64:7; Warumi 3:19, 20). Sisi kama wanadamu ni udongo, hatuwezi kudumu kwa muda mrefu, kama mdudu. Na ni nani anayeweza kuwa na haki kuliko Mungu?
Kwa upande mwingine maneno yake yalikuwa hayana maana na yalikuwa nje ya suala la msingi. Tatizo la Ayubu halikuwa kama Ayubu alikuwa bora kuliko Mungu au la. Hilo halikuwa lalamiko la Ayubu. Zaidi sana alizungumzia hali mbaya aliyokuwa nayo, namna alivyokuwa anateseka, si kwamba kwa kiasi fulani alikuwa na haki kuliko Mungu.
Hata hivyo, Elifazi, anaonekana kuyaona yote haya kutoka kwenye maneno ya Ayubu. Kwanza, kama Mungu ni mwenye haki, na kwamba mabaya huwakuta wale walio waovu tu, basi ni lazima kwamba Ayubu alistahili yale mambo aliyokuwa anayapitia. Kwa hiyo malalamiko ya Ayubu hayakuwa ya haki. Akiwa amedhamiria kumtetea Mungu, Elifazi anaanza kumpa somo Ayubu. Zaidi ya ujuzi wo wote wa pamoja aliokuwa anadhani anao juu ya Mungu, Elifazi alikuwa na jambo lingine: ufunuo wa aina fulani usiokuwa wa kawaida kuunga mkono hoja yake. Hata hivyo, tatizo pekee ni kwamba hakulielewa tatizo.
Tunaweza kujifunza nini kutoka katika maelezo haya juu ya jinsi tunavyoweza kushindwa kuelezea hoja kwa njia inayoweza kusaidia na kukomboa, hata kama tuko sahihi juu ya hoja husika?
No comments:
Post a Comment