Dhambi Imesamehewa, Makosa Yamesitiriwa
Heri aliyesamehewa dhambi, na kusitiriwa makosa yake. Zaburi 32:1.
Kwamba Mungu anayetambua shomoro akianguka, anaona mwenendo na hisia zetu; anatambua kijicho chako, kiburi chako, unavyojaribu kuhalalisha kitendo chako katika suala dogo kabisa lisilo haki. Unapokuwa hujaelewa maneno na matendo ya mwingine kwa usahihi na wakati hisia zako mwenyewe zinapokuwa zimechokozwa, kiasi cha wewe kutoa kauli zisizo sahihi na inajulikana kwamba umetofautiana na ndugu yako, unaongoza wengine, kwa njia ya imani yao kwako, kumuona kama wewe umwonavyo; na kutokana na mzizi wa uchungu unaoota, wengi wanachafuliwa. Inapokuwa dhahiri kwamba hisia zako haziko sahihi, je, unajaribu kwa bidii kuondoa mitazamo iliyokosewa kama ulivyojitahidi katika kuionesha?...
Sasa, Mungu anakutaka wewe ambaye umetenda isivyo haki katika lile lililo dogo kabisa kwa mtu mwingine, kwamba ukaungamie kosa lako, siyo tu kwa yule uliyemuumiza, bali pia kwa wale ambao kupitia kwa mvuto wako wamefanywa kumwona ndugu yao katika mwonekano usio mzuri na kuifanya kazi ambayo Mungu amempatia aifanye kutokuwa ya maana… Kwa kutubu na kuungama unaweza kuandikiwa msamaha katika jina lako; au unaweza kukataa ushawishi wa Roho wa Mungu na kwa sehemu inayosalia ya maisha yako ukafanya kazi ukifanya ionekane kwamba hisia zako ambazo hazikuwa sahihi na mahitimisho yasiyo ya haki visingeweza kubadilishwa. Lakini, tendo linasalia limesimama, uovu uliotendwa unasalia, uharibifu wa wale ambao mioyoni mwao umepandikizwa mizizi ya chuki…..
Bila kujali aina ya dhambi yako, iungame. Ikiwa ni dhidi ya Mungu mwenyewe, iungame kwake tu. Ikiwa kwa makosa umewakwaza wengine, waungamie hao pia na baraka ya Bwana itakuwa juu yako. Kwa njia hii unaifia nafsi na Kristo anaumbwa ndani yako… Kujitoa kwetu kwa Mungu lazima kusizuie chochote, upendo wetu ukiwa wenye shauku, imani yetu ikiwa ile isiyoyumba. Ndipo kauli za midomo yetu zitashuhudia juu ya wepesi wa akili na mguso wa ndani zaidi wa Roho wa Mungu kwenye nafsi ya mtu.

No comments:
Post a Comment