Mwili wa Fidel Castro kuchomwa
Cuba inaadhimisha siku tisa za maombolezo kufuatia kufariki kwa Fidel Castro, anayejulikana kwa siasa zake za kimapinduzi, aliyetawala taifa hilo kwa miongo kadhaa na ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 90.
Mwili wake, utachomwa hadi kuwa majivu kama alivyotaka, katika sherehe ya kibinafsi, ambapo majivu yake yatazungushwa katika msafara maalumu kote nchini kabla ya kuzikwa katika Makaburi ya Mji wa Santiago Desemba tarehe nne.
Akiwa kiongozi mwenye mrengo wa kushoto na mwanamapinduzi msifiwa, alipendwa na kuchukiwa na watu mbalimbali kote duniani.
Watu wengi katika mji mkuu wa Havana walidondokwa na machozi kwa kuwa kiongozi shujaa aliyeweza kukabiliana na Marekani katika uwanja wa kidiplomasia kwa miongo kadhaa, licha ya mbinu nyingi zilizofanywa za kutaka kumuua.
Waasi wa Serikali ya Castro hata hivyo walisherehekea kote duniani, walikotorokea.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment