Fidel Castro: Magufuli na Kenyatta watuma rambirambi
mwenzako
Rais wa Tanzania John Magufuli amemtumia salamu za rambirambi rais wa Cuba Raul Catsro kufuatia kifo cha rais mstaafu wa Cuba Fidel Castro.
Katika salamu hizo magufuli amesema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Fidel Castro.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Magufuli amesema kuwa kwa niaba yake pamoja na wananchi wa taifa la tanzania ametoa pole kwa wananchi wa Cuba kwa kumpoteza mtu muhimu.
Amemsifu Fidel kwa kuwa kiongozi sahupavu ambaye atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika ukombozi wa nchini za Kusini mwa Afrika pamoja na misaada mikubwa aliyotoa kuboresha huduma zas kijamii kwa wananchi.
''Alikuwa rafiki wa Tanzania na Afrika nzima,historia ya Tanzania haiwezi kukamilika bila kumtaja Fidel Castro .
Hakika kifo chake sio tu ni pigo kw Cuba bali pia kwa Tanzania na Afrika'',alisema Magufuli.
Wakati huohuo rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa ulimwengu umempoteza mpigania uhuru,kiongozi na mzalendo.
Amesema kuwa Fidel Castro alifanikiwa kuongoza mapinduzi kutokana na msukumo wake wa kuamini kuhusu usawa na maendeleo ya Cuba.
Anasema kuwa wakati wa ugonjwa wa Ebola barani Afrika ,Castro aliwatuma madaktari kuja kuwatibu waliothirika na ugonjwa huo barani Afrika.
Amemuomba muungu kuiweka roho yake mahali pema peponi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment