Geert Wilders: Mashitaka yangu yanachochewa na chuki za kisiasa
Geert Wilders ambaye ni Kiongozi wa chama tawala, kinachopinga uislam nchini Uholanzi ameiambia mahakama kwamba mashtaka yake yanachochewa na chuki za kisiasa chafu pamoja na ubaguzi wa rangi.
Katika kipindi cha Televisheni alipokuwa akisomewa mashtaka yake mara ya mwisho, ameeleza kuwa mahakama haitamhukumu yeye peke yake bali itawahukumu mamilioni ya wanaume kwa wanawake nchini Uholanzi.
Kiongozi huyo amesema ana haki ya kuongelea matatizo ya nchi hiyo ikiwemo kupunguza idadi ya wananchi wa Morocco wanaoishi nchini humo.
Mashtaka hayo yamesababishwa na uchochezi wa kiongozi huyo ambapo alisikika akiwauliza wafuasi wake kama wanataka idadi ndogo ya wamorocco wanaoishi Nchini humo huku wafuasi wake walisikika wakishangilia na kujibu, idadi chache! Chache!
Uholanzi inatarajia kufanya uchaguzi mkuu mwezi wa tatu mwakani na baadhi ya kura za maoni zinapendekeza bwana Wilders, na chama cha uhuru kikiongoza.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment