» »Unlabelled » ZITTO – KIGOMA MJINI ITAKUWA MFANO 2020

ZITTO – KIGOMA MJINI ITAKUWA MFANO 2020

 

Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto kupitia chama cha ACT-Wazalendo amesema chama chake kimeweka malengo kadhaa ya kuifanya Manispaa ya Kigoma Ujiji kuwa ya mfano ifikapo 2020. “Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015, tulieleza malengo yetu kwa wananchi, huu ni mwaka wa kwanza wa bajeti na mambo mengi yanafanyiwa kazi, bado kuna changamoto za utekelezaji wa malengo tuliyojiwekea,” amesema.

Anapozungumzia miundombinu, Zitto amesema mbali na ujenzi wa barabara zilizo chini ya Tanroads na zile zilizo katika ahadi ya Rais, Manispaa hiyo imekubaliana na Shirika la BTC la Ubelgiji kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa mitaa ya mawe katika kata nane. Pia amesema zabuni ya kujenga mzunguko wa eneo la Mwanga Sokoni tayari imetangazwa na kufunguliwa na ujenzi unaanza mwaka wa fedha 2016/17.ZITTO KABWE“Malengo ya kujenga mifereji katika mitaa ya manispaa, barabara za lami na mawe, kujenga daraja Mto Luiche na barabara kata ya Kagera kutokea Ujiji, mkandarasi ameanza kazi ya kukusanya vifaa,” amesema.

Alisema pia Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unaanza ujenzi wa Soko la Mwanga ambapo ndani yake kutakuwa na mnada wa kimataifa wa asali, ujenzi utakaofuatiwa na uboreshwaji wa soko la mjini Kigoma ambalo litajengwa maduka makubwa.

ZITTO KABWE

“Soko la Ujiji lina mradi maalumu wa kujenga Kituo cha Kikanda utakaotokana na uwekezaji kutoka nchini China utawezesha ujenzi wa maduka 3000, warehouses (magodauni) na nyumba za makazi. Mradi huu ni kuiwezesha Ujiji kuwa eneo la wananuzi wa bidhaa kutoka nchi za Maziwa Makuu badala ya watu hao kusafiri kwenda Mashariki ya Mbali,” amesema.

 Chanzo.  MTEMBEZI.COM

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles