» »Unlabelled » Wakimbizi walalamikia hali mbaya inayowakabili Daadab

Wakimbizi walalamikia hali mbaya inayowakabili Daadab


Jubaland kwa sasa imekataa kupokea wakimbizi zaidi
Image captionJubaland kwa sasa imekataa kupokea wakimbizi zaidi
Maelfu ya wakimbizi wa Somalia wamekwama katika kambi ya Dadaab Refugee kaskazini mashariki mwa Kenya baada ya jitihada za kuwarudisha nyumbani kusitishwa takriban mwezi mmoja uliopita.
Utawala wa Jubaland nchiniSomalia umekataa kupokea wakimbizi hao kufuatia mzozo na Shirika la Umoja wa mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNCR na serikali ya Kenya.
Hivi sasa baadhi ya wakimbizi wameiambia BBC kwamba wameuza mali zao tayari kurudi nyumbani na sasa hawana mahali pa kwenda.
Hawa Mohamed Muse ni mmoja wa wakimbizi waliokwama. '' Hatuna chakula, kuna baridi usiku na hatuna mahali pa kujihifadhi.
Baadhi wanasema wanatumia nguo kujiking ana baridi
Image captionBaadhi wanasema wanatumia nguo kujiking ana baridi
''Tunaishi chini ya miti, tunapata chanjo tu kwa watoto wetu lakini hakuna dawa kwa watu wazima. Hatuna mipango yoyote tunasubiri tu kauli ya Umoja wa mataifa", anasema Hawa.
Haya yanatokea wakati viongozi wa dunia wanakutana New York katika kikao maalum kuuhsu mzozo wa wakimbizi duniani.
Msemaji wa UNHCR ameiambia BBC kwamba wanawashughulikia wakimbizi 2000 waliopo katika kituo cha muda wakisubiri kuanza upya mpango wa kurudisha nyumbani. Amekana kuwa wakimbizi hao wapo katika hali mbaya.
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU WATARIFU NA WENZAKO PIA TUPIA MAONI YAKO

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles