» »Unlabelled » Progamu ya Windows 10 lawamani

Progamu ya Windows 10 lawamani


Mkurungezi mtendaji mkuu wa Microsoft Satya NadellaImage copyrightAP
Image captionMkurungezi mtendaji mkuu wa Microsoft Satya Nadella
Kampuni ya Microsoft imeshtumiwa na kundi la haki za wateja la Consumer Rights dhidi ya programu yake ya Windows 10.
Kundi hilo limesema limepokea mamia ya malalamishi kuhusiana na uboreshaji wa programu hiyo .
Watumiaji wa programu hiyo wanalazimika kulipia komputa zao ili zirekebishwa kutokana na faili kupotea.
Hatahivyo Microsoft ilitetea programu hiyo ya Windows 10 na kusisitiza kuwa imekuwa ikitoa usaidizi kupitia mtandaoni na vilevile kwa simu.
Imeongezea kwamba itawasaidia watu kupata programu yenye manufaa na yenye usalama dhabiti, kulingana na msemaji wa kampuni hiyo.
Programu ya Windows 10 hutumika kwa simu aina ya smartphoneImage copyrightTOBIAS SCHWARZ
Image captionProgramu ya Windows 10 hutumika kwa simu aina ya smartphone
Kundi hio limesema watumiaji wamekuwa wakilalamikia ujumbe uliokuwa ukijitokeza kwenye tarakilishi na simu zao kila mara, kuwahimiza kuboresha programu hiyo mbali na programu hiyo ya Windows 10 kujiweka yenyewe bila idhini ya mtumiaji.
Pia kumekuwa na malalamiko kuhusiana na huduma mbaya kwa wateja wake,pale wanapohitaji msaada kutoka kwa kampuni hiyo.
Programu hiyo ya windows 10 ilizinduliwa mwezi Julai mwaka 2015, na hutumika katika tarakilishi,simu aina ya smartphone, na vifaa vya kusikilizia sauti vya HoloLens.
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU WATARIFU NA WENZAKO PIA TUPIA MAONI YAKO

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles