» »Unlabelled » Makombora ya Muungano wa Saudia yawaua 19 Yemen

Makombora ya Muungano wa Saudia yawaua 19 Yemen


Afisa wa serikali Yemen anasema huenda makaazi ya watu yalilengwa 'kimakosa'Image copyrightREUTERS
Image captionAfisa wa serikali Yemen anasema huenda makaazi ya watu yalilengwa 'kimakosa'
Raia 19 wameuawa katika mji wa bandari wa Hudaydah nchini Yemen kwenye mashambulio ya muungano unaoongozwa na Saudia, maafisa wa eneo hilo na wahudhumu wa afya wanasema.
Uvamizi wa jumatano unaarifiwa kulenga kasri la rais linalotumika na waasi wa Houthi lakini makombora yalilenga nyumba zilizokaribiana na kasri hilo.
Wakaazi wameilezea uharbifu mkubwa uliotokea katika wilaya ya al-Hunoud.
Muungano huo, unaotaka kuirudisha uongozini utawala unatoambulika kimataifa ya Yemen, bado haujatoa kauli.
Maafisa wa muungano huo wanasema hulenga maeneo ya kijeshi pekee, lakini umeshutumiwa kwa kulenga shule, hospitali, masoko na makaazi ya watu tangu kuingilia kati mzozo wa Yemen miezi 18 iliopita.
Shirika la habari la Saba linalodhibitiwa na waasi limeripoti kuwa nyumba kadhaa ziliharibiwa katika shambulio hilo la Hudaydah.
Hali imekuwa mbaya Yemen na watu wengi wanahitaji usaidizi wa kibinaadamuImage copyrightREUTERS
Image captionHali imekuwa mbaya Yemen na watu wengi wanahitaji usaidizi wa kibinaadamu
Imetaja wahudumu wa afya waliosema kuwa kuna watu 98 waliofariki wakiwemo wanawake na watoto.
"kulikuwa na uharibifu mkubwa. Sehemu za mwili zimechangika na masalio ya nyumba zilizoporomoka na damu imetapakaa kila mahali," mkaazi mmoja ameliambia shirika la habari la Reuters.
Afia wa serikali ameliambia shirika la AFP kwamba eneo hilo la makaazi huenda limelengwa 'kimakosa'.
Umoja wa mataifa unasema zaidi ya watu 6, 700 wameuawa tangu kuanzishwa kwa kampeni ya kijeshi inayomuunga mkono rais Abdrabbuh Mansour Hadi Machi 2015, miezi mitatu baada ya waasi kuudhibiti mji mkuu, Sanaa.
Mzozo huo pia umeisukuma nchi hiyo masikini katika mataifa ya kiarabu karibu kuingia kwenye baa la njaa na kusababisha 80% ya idadi ya watu nchini humo kuhitaji usaidizi wa kibinaadamu.
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU WATARIFU NA WENZAKO PIA TUPIA MAONI YAKO

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles