» »Unlabelled » Wafungwa wagoma wakitaka malipo Australia

Wafungwa wagoma wakitaka malipo Australia


Mshirikishe mwenzako
Jela ya Barwon nchini AustraliaImage copyrightALAMY
Image captionJela ya Barwon nchini Australia
Wafungwa katika jela moja nchini Australia wamegoma wakidai malipo.
Wafungwa wote katika jela ya Barwon mjini Victoria wanahitajika kufanya kazi isipokuwa wanapokuwa wagonjwa sana ama wakati wanapokuwa wazee sana .
Wafungwa waliogoma wanasema kuwa dola 6.90 walizoahidiwa katika makubaliano mapya hazitoshi kusimamia gharama yao ya maisha.
Upinzani nchini humo unataka walazimishwe kurudi kufanya kazi ,ukisema kuwa wananchi wamekasirishwa na hatua kwamba wafungwa hao wana uwezo wa kugoma.
Malipo ya dola 9 kwa siku ambayo wafungwa hao wameahidiwa ,kulingana na kazi zao na saa wanazofanya kazi ,ni ongezeko la malipo ya sasa ya kati ya dola 6.50 na dola 8.95,lakini imekosolewa kutotosha na wafungwa na wafuasi wao.
Malipo hayo ni ya kiwango cha chini sana ikilinganishwa na majimbo mengine nchini Australia na hayafikii gharama zao zinazoongezeka kila uchao,alisema Brett Collins,msemaji wa kundi linalopigania haki za wafungwa.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles