» »Unlabelled » Kiongozi wa Ufilipino Duterte asema hakukusudia kumshambulia Obama

Kiongozi wa Ufilipino Duterte asema hakukusudia kumshambulia Obama

Mshirikishe mwenzako
Rodrigo DuterteImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionWatu 2,400 wameuawa katika vita dhidi ya mihadarati tangu Rais Rodrigo Duterte aingie madarakani Juni
Kiongozi wa Ufilipino Rodrigo Duterte amesema anajutia kwamba amatamshi yake kumhusu kiongozi wa Marekani Barack Obama yamefasiriwa kama matusi.
Bw Duterte amesema hayo baada ya Bw Obama kufuta mkutano wake na kiongozi huyo kutokana na maneno ya lugha chafu yaliyoelekezwa kwake.
Kiongozi huyo wa Ufilipino alikuwa amemweleza Bw Obama kama "mwana wa kahaba" na kuongeza kwamba hatakubali kuulizwa maswali kuhusu ukiukwaji wa haki za kibinadamu nchini mwake.
Alisema Ufilipino haitawaliwi na mtu yeyote. Ufilipino ilikuwa koloni ya Marekani.
Hayo yalijiri kabla ya kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa nchi za Kusini Mashariki mwa bara Asia, mjini Laos.
Lakini kupitia taarifa, Bw Duterte amesema anajutia matamshi hayo.
Amesema wanadiplomasia wa Ufilipino na Marekani wanatarajia kuondoa uhasama na tofauti zilizozuka baina ya nchi hizo mbili.
Barack ObamaImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionRais Barack Obama alionywa na Bw Duterte "kuonyesha heshima"
Tangu kuingia madarakani, Bw Duterte ameendelea kutumia maneno makali, na kutumia lugha chafu kuwarejelea Papa Francis, maafisa kadha wa Umoja wa Mataifa, waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na balozi wa Marekani nchini Ufilipino.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles