» »Unlabelled » Wachezaji wa El Salvador wakataa hongo

Wachezaji wa El Salvador wakataa hongo


wenzako
Wachezaji wa timu ya taifa la El salvador
Image captionWachezaji wa timu ya taifa la El salvador
Wachezaji wa timu ya taifa ya El Salvador wanasema kuwa wamekataa kuchukua hongo ili wakubali kushindwa katika mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya Canada siku ya Jumanne.
Katika mkutano na vyombo vya habari,wachezaji wa timu hiyo walicheza sauti ya mtu aliyejaribu kuwahonga kupitia kuwapatia zawadi kadhaa.
Canada ni sharti iishinde El Salvador huku wakitumai kwamba Mexico itaishinda Honduras katika fainali ya mechi ya kimakundi ili kuwa na fursa ya kuendelea.
El Salvador haiwezi kufuzu katika ya raundi ya mwisho ya kimakundi.
''Ni kisa kisicho cha kawaida kuweza kutokea'' ,alisema mwandishi mpekuzi wa BBC Declan Hill.
Zawadi kuu ambayo wangepata ni dola 3,000 kwa kila mchezaji.
Timu yote ilijitokeza na kocha wake na kusema kuwa walijaribiwa kuhongwa siku ya Jumamaosi.
Walicheza sauti ya dakika 11 ya mtu aliyejaribu kufanya uovu huo.
Hill anasema kuwa hongo hiyo ilidaiwa kutolewa na raia wa El Salvador ambaye anawajua baadhi ya wachezaji,lakini ambaye alitaka kukisaidia kikosi cha Honduras.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles