» »Unlabelled » Serikali yasema usalama wa nchi unaendelea kuimarishwa

Serikali yasema usalama wa nchi unaendelea kuimarishwa
Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amesema usalama wa wananchi utaendelea kuimarishwa huku serikali ikidhibiti vitendo vya mauaji ya raia na askari
Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amesema usalama wa wananchi utaendelea kuimarishwa huku serikali ikidhibiti vitendo vya mauaji ya raia na askari katika maeneo mbali mbali hapa nchini.

Waziri Mkuu MAJALIWA ameyasema hayo katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mbunge wa Korogwe STEVEN NGONYANI kuwa serikali itaimarisha ulinzi zaidi na inaendelea kuwasaka wale wote wanaohusika na vitendo hivyo viovu.

Waziri Mkuu MAJALIWA amesema serikali imesikitishwa na vitendo vya mauaji vinavyoendelea na kwamba  vyombo vya dola vipo macho kuimarisha ulinzi katika maeneo yote.

Akijibu maswali ya Papo kwa papo Bungeni mjini DODOMAWaziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amesema lengo la serikali ya awamu ya TANO ni kuhakikisha uchumi wa nchi unakuwa.
Kuhusu suala la tozo katika zao la korosho Waziri Mkuu MAJALIWA amesema zao hilo lina matatizo mbali mbali ikiwemo stakabadhi ghalani na wanunuzi kwenda kwenye minada wakiwa hawana fedha.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles