» »Unlabelled » IGP MANGU kukabidhiwa uenyekiti SARPCCO

IGP MANGU kukabidhiwa uenyekiti SARPCCO
Mkuu wa jeshi la polisi nchini Inspekta Jenerali wa Polisi IGP ERNEST MANGU anatarajia kukabidhiwa uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Majeshi ya Polisi
Mkuu wa jeshi la polisi nchini Inspekta Jenerali wa Polisi IGP ERNEST MANGU
Mkuu wa jeshi la polisi nchini Inspekta Jenerali wa Polisi IGP ERNEST MANGU anatarajia kukabidhiwa uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Majeshi ya Polisi kusini mwa Afrika, SARPCCO wakati wa mkutano utakaofanyika Septemba 16 mwaka huu jijini Arusha.

Kwa mujibu wa tarifa iliyotolewa na jeshi la polisi nchini, IGP MANGU atakabidhiwa uenyekiti huo kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la MSUMBIJI na atadumu katika nafasi hiyo kwa mwaka mmoja.

Tarifa hiyo imeeleza kuwa Mkutano huo utatanguliwa na mkutano wa siku mbili wa kamati tendaji za SARPCCO ambazo zitaandaa ajenda na mapendekezo  yatakayowasilishwa katika mkutano wa wakuu wa Polisi.
Mkutano huo pamoja na mambo mengine utajadili namna ya  kukabiliana na uhalifu wa kuvuka mipaka na kuweka mikakati na maazimio ya kufanya Oparesheni za pamoja za kupambana na uhalifu
Pia  mkutano huo utajadili utekelezaji wa maazimio mbalimbali kupitia kamati tendaji za wakurugenzi  wa upelelezi, kamati tendaji ya sheria, kamati tendaji ya mafunzo na kamati tendaji ya mtandao wa Polisi wanawake.
SARPCCO iliundwa mwaka 1995 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa Majeshi ya Polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika katika kukabiliana na uhalifu yenye nchi KUMI na TANO ikiwemo TANZANIA

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles