Kwa Picha: Mvuto wa Botswana
nzako
Huu ni mkusanyiko wa picha za maeneo ya kuvutia pamoja na wanyama pori nchini Botswana. Picha hizi zilipigwa na watu mbalimbali na zinaashiria mvuto ambao huwafanya watalii kutembelea taifa hilo la kusini mwa Afrika kwa wingi.
- Anna Sobotka, ambaye ni mara yake ya kwanza kufika Afrika, anasema: "Sikutarajia kupendezwa na umaridadi na mandhari ya taifa hili kama nilivyofanya." Alipiga picha hii ya ndovu wakioga Mbuga ya Taifa ya Wanyama ya Chobe
- Hii ni picha nyingine kutoka Mbuga ya Taifa ya Wanyama ya Chobe, wakati huu kutoka kwa Anne May ambayo inawanesha twiga wakinywa maji mto Chobe
- Ndege hawa aina ya Roller wanaonyesha rangi za kupendeza ambao mtalii hukumbana nazo anapotembea porini Botswana. "Ndege hawa hupendeza wakiwa kwenye miti, lakini zaidi wakippaa na kupita mbele yako," anaandika Philip Willmott
- Kuna mibuyu ya kuvutia pia. Mibuyu inayokua Botswana baadhi ilimea karne nyingi zilizopita.
- Mshiriki wa mashindano ya mbio za magari jangwani katika Jangwa la Kalahari mwaka 2015, mashindano yanayofanyika kila mwaka.
- Jua likitua Okavango Delta.
- Mnyama ajulikanaye kama meercat aonekana jua likitua eneo la Makgadikgadi Pans, moja ya maeneo tambarare yenye chumvi nyingi zaidi.
- Hapa ni maeneo ya kaskazini ya Okavango Delta eneo lifahamikalo kama NG23 karibu na Seronga.
- Wanyama wanapatikana kwa wingi. Chui huyu alipigwa picha na Kim Pickett Mbuga ya Taifa ya Wanyama ya Chobe. Botswana ina wanyama wakubwa wengi zaidi wa jamii ya paka kusini mwa Afrika.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:
Post a Comment