» »Unlabelled » Idadi yaongezeka waliokufa katika ajali ya boti Misri

Idadi yaongezeka waliokufa katika ajali ya boti Misri


Mshirikishe mwenzako
Wahamiaji njiani kuelekea UlayaImage copyrightAP
Image captionWahamiaji njiani kuelekea Ulaya
Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya boti iliyokuwa imebeba wahamiaji haramu wanaokadiriwa kufikia mia sita, iliyozama nje kidogo ya pwani ya Misri imeongezeka na kufikia 42.
Mamlaka nchini humo zinasema mpaka sasa watu wengine laki moja na hamsini wameokolewa.
Mmoja wa ndugu wa wahamiaji hao waliokuwa ndani ya boti Hassan Suleiman Daoud, amezitupia lawama, mamlaka nchini Misri kwamba zilikuwa zikishughulikia tatizo hilo taraatibu.
''...Tuliziambia mamlaka husika tangu majira ya saa kumi na moja na nusu kwamba boti inazama, lakini walikuwa wakisema hakuna boto ya uokoaji, na hakuna aliyekuwa akishughulikia...'' alisema Hassan.
Amefahamisha pia kwamba boti zao za uvuvi ndizo zilikuwa zikifanya kazi ya kuitafuta boti hiyo na kuokota maiti baharini na watoto pia kutoka ndani ya maji.
Amefahamisha pia kwamba wafanyabiashara haramu ya wahamiaji, wanatambuliwa na polisi katika maeneo haya pia amelaumu kuwa huchukua malipo ya mwezi kutoka kwao.
Katika kipindi cha mwaka huu pekee, wahamiaji wapatao laki tatu wamekatisha bahari ya Mediteranea na kuingia barani Ulaya, lakini njia yao kubwa ni ile ya kutokea Libya.
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU WATARIFU NA WENZAKO PIA TUPIA MAONI YAKO

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles